Vidokezo za Karatasi ya Pili

YALIYOMO KATIKA KARATASI YA PILI.

 • Ufahamu
 • Ufupisho.
 • Matumizi ya lugha
 • Isimujamii.
  • Ufahamu ni sehemu ya mtihani wa karatasi ya pili.
  • Mtahiniwa hupewa kifungu cha meneno anayotakiwa kusoma kwa umakinifu mkubwa.
  • Yapo maneno mapya ambayo mtahiniwa atajifunza kutoka kwayo.
  • Yapo maswali mengine yanayoulizwa katika maswali ya ufahamu ambayo yapo nje na ufahamu aliosoma.
  • Maswali haya madhumuni yake ni kujaribu uwelewa wa mtahiniwa katika nyanja ya lugha ya Kiswahili.
  VIDOKEZO!
  • Baada ya kusoma kwa makini, atatakiwa kujibu maswali yanayohusiana na ufahamu aliousoma.
  • Kumbuka asilimia kubwa ya maswali ya ufahamu majibu yake yamo katika ufahamu.
  • Kutokana na neno ufupisho tunapata, ‘’fupisha’’ yaani punguza kitu kilichokua kirefu na kuwa kifupi na kinachoeleweka.
  • Katika swali la ufupisho, mtahiniwa hupewa ufahamu mrefu asome na kuuelewa.
  • Baada ya kusoma na kuuelewa kwa mapana, atatakiwa kufupisha maneno aliyoyasoma hadi kiwango ambacho ataulizwa katika maswali.
  • Sehemu ya matayarisho pia huitwa nakala chafu.
  VIDOKEZO!
  • Mtahiniwa anatakiwa kuzipanga hoja zake zote zilizo bayana.
  • Unapoambiwa kua hio ni nakala chafu, ina maana ya kua hio ni nakala inayotengenezwa ili kutaarisha nakala iliyo safi.
  • Hivyo basi itamhitaji mtahiniwa kupiga mstari wa mshazari (/) ili kuyafuta yale aliyoandika.
  • Sehemu ya matumizi ya lugha ndiyo inayobeba asilimia kubwa ya alama katika mtuhani wa karatasi ya pili.
  • Hua na alama zinazofikia arobaini (40).
  • Maswali ya matumizi ya lugha humzindua mwanafunzi kwa kuuliza maswali yanayogusia muundo na msingi wa lugha ya Kiswahili.
  VIDOKEZO!
  Baadhi ya maswali ni kama vile;
  • Sauti za matamshi – huuliza kuhusu suati za matamshi, sifa zake na sehemu zipotamkiwa.
  • Methali na nahau. – huuliza methali ili mtahiniwakukamilisha. Pia huuliza maana za nahau.
  • Umoja na wingi—huuliza kuhusu kugeuza sentensi katika umoja au wingi.
  • Uakifishaji.—hutahini kuhusu alama za uakifishaji na matumizi yake.
  • Maswali ya misamiati.—huuliza maneno au majina mapya na maana yake.
  • Ukubwa na udogo.—humhitaji mtahiniwa kubadilisha sentensi katika ukubwa au udogo.
  • Aina za maneno.—huuliza kuhusu aina nane za maneno ; nomino, kivumishi, kihusishi,kihisishi, kielezi,kiunganishi, kiwakilishi na kitenzi.
  • Ukanusho na kinyume.-- kukanusha ni kukataa na kinyume ni tofauti ya jambo.
  • Ngeli za majina. – huuliza kuhusu ngeli faaafu za majina. Ujuzi wa ngeli sahihi humsaidia mtahiniwa jinsi ya kuzungumza kwa ufasaha.
  • Uchanganuzi wa sentensi. – humhitaji mtahiniwa kuivunja sentensi ili kupata aina za maneno kwa kutumia mbinu kama vile; matawi, mtari, mshale na jedwali.
  • Mnyambuliko wa vitenzi n.k – huuliza kuhusu jinsi neno linavyoweza kunyambuliwa kwa vitenzi katika kauli kama vile; kutenda, kutendana, kutendatenda, kutendua, kutendwa, kutendeka ,kutendesha , na nyengine nyingi.
  • Uyanishaji – humhitaji mtahiniwa kuirudisha sentensi kutoka hali ya ukanusho hadi hali ya sawa.
  • Isimujamii ni taaluma inayochunguza lugha na matumizi yake katika jamii.
  • Lugha huweza kuchunguzwa kutokana na utofauti wake na lugha nyenginezo baada ya kufanya ulinganishi.
  • Vilevile isimujamii huchunguza ni kwanini mawasiliano baina ya watu yanaweza kufanyika ila watu wasielewane.
  VIDOKEZO!
  • Mtahiniwa anaweza kupewa dondoo kisha akaulizwa abainishe sajili, hii ina maana ya kua, aeleze ni sehemu gani ambapo lugha hio inatumika.
  • Ni vizuri atoe sababu kutokana na dondoo hio.
  • Iwapo atasema sajili ni ya sokoni, basi mtahiniwa anafaa kuonyesha ithibati kutoka kwenye kifungu cha maneno alichopewa na kuthibitisha jibu alilotoa.
  Scroll to Top