Kenglex ni kamusi ya tafsiri ya Kiswahili na Kiingereza, haswa kile Kiingereza kinachozungumzwa nchini Kenya.  Ule mwelekeo tuliochukua ni kuwa, hicho Kiingereza hakiwezi kukamilika bila kutumia maneno mengi ya asili, na pia ya Kiswahili. Tukaona hatuwezi kutenganisha Kiingereza na Kiswahili, na kwa hivyo tukaongeza maneno yote ya Kiswahili kwa msamiati.

KENGLEX ni kamusi ya utafiti iliyo na malengo mengi. Baadhi ya malengo haya, ni kama vile:

 • Kuongeza matini ya utafiti katika vitengo vya elimu na utafiti.
 • Kukuza lugha duniani kote.
 • Kufahamisha ulimwengu kuhusu lahaja ya Kiingereza cha Kenya.
 • Kuhifadhi lugha ya Kiswahili kutokana na mwingiliano wa lugha nyengine.
 • Kuongeza misamiati mipya kutokana na mwingiliano wa lugha nyengine.
 • Kusaidia katika kutafsiri na kuboresha matamshi.

Mbali na hayo, KENGLEX ni kamusi ya kiutofauti kwa sababu ina vipengee muhimu ambavyo vitaweza kumsaidia mtafiti au mpenzi yeyote wa lugha.

 • Mwanzo kabisa, maneno yametofautishwa kwa wino. Maneno ya Kiswahili yapo katika wino wa kijani, na maneno ya Kiingereza yapo kwa rangi ya samawati.
 • Kila neno limepewa aina yake (part of speech), ima, nomino au noun, kitenzi au verb, kielezi au adverb, ama aina yeyote-ile kwa lugha zote mbili
 • Maana ya meneno yote ni katika lugha ya Kiingereza.
 • Kila neno limepewa fonetiki zake ili mtu aweze kujua vipi litakavyo tamkwa.
 • Kila neno lina mtamko wa sauti inayosikika kwa ufasaha, na katika lugha zote mbili. Hii itaweza kumsaidia mtu yeyote atakayepata ugumu wa kulisoma neno.
 • Maneno yanayohusiana yameorodheshwa katika kiorodhesho kilicho juu ya neno.
 • Maneno ya Kiswahili yamepewa visawe kwa lugha ya Kiingereza, na yale ya Kiingereza yamepewa visawe kwa lugha ya Kiswahili. Visawe hivi vimeorodheshwa katika kiorodhesho kilicho chini ya neno.
 • Pia, maneno mengine yamepewa wingi wake na kuorodheswa katika kiorodesho cha juu.

Kupitia kamusi hii ya kimtandao, itaweza kuwafikia watu wengi katika mataifa mengi kwa sababu, hivi sasa tupo katika ulimwengu wa utandawazi. Watalii watakao kuja zuru Afrika Mashariki hawatopata ugumu wa kuzungumza. Taasisi za utafsiri vilevile, zitakua zimeongeza matini mapya ya utafsiri. Mzungumzaji wa lugha, hatopata ugumu wa kuzungumza endapo atakua na KENGLEX anayoimiliki katika simu yake. Kupitia teknolojia na ufundi uliotumika kuiunda, utumizi wa kamusi hii utakua wa haraka na rahisi, kila wakati na kila mahali.

Teknobyte Limited

Teknobyte Limited (www.teknobyte.ltd) is an East African-based technology company that develops and provides Engineering and ICT solutions in various sectors within the greater region. Teknobyte was founded in 1994 and operated as a business until 2002, when we incorporated it as a limited liability company.

We have been researching Spoken Language Technologies since 2004 when we developed the first Text-to-Speech Systems (TTS) in local languages: the Kiswahili TTS and the Kenyan English TTS. We subsequently applied these products to the development of NAFIS – the National Farmers Information Service, an innovative and comprehensive farmers’ information service launched in April 2008. NAFIS integrated the internet and speech technologies systems to realize a flexible, readily updated voice and an interactive web service for agricultural extension.

To develop the Kenyan English TTS, we defined and authenticated the language features and built them into a 60,000-word pronunciation dictionary. We then improved the intonation features of the Kiswahili TTS by incorporating questions into the system, among other features. The Kenyan Languages Lexicon Project is building on this work to bring these innovations for use by the large public.

Scroll to Top