Karatasi ya kwanza ya Kiswahili humhitaji mwanafunzi kutumia ubunifu wake mkubwa wa kuandika pamoja na umbuji wa hoja na mawazo yaliyo na ustadi mkubwa.
Karatasi ya kwanza hua na maswali manne, ambapo swali la kwanza ni la lazima. Maswali yamayofuata ni maswali ya hiari. Hivyo basi itamlazimu mtahiniwa kufanya maswali mawili pekee.
VIDOKEZO!
Sura ya insha zote za kiuamilifu. Lazima afahamu umbo la kila aina ya insha.
Urefu wa insha yake. Maneno yasiwe mengi Zaidi au machane yawe takriban maneno 400
Azingatie nyakati kulingana na aina ya insha.
Azingatie cheo na nyadhifa ya kila mhusika atakaye muandika katika insha yake.
Azingatie vyema alama za uakifishaji.