Vidokezo za Karatasi ya Pili
YALIYOMO KATIKA KARATASI YA PILI.
- Ufahamu ni sehemu ya mtihani wa karatasi ya pili.
- Mtahiniwa hupewa kifungu cha meneno anayotakiwa kusoma kwa umakinifu mkubwa.
- Yapo maneno mapya ambayo mtahiniwa atajifunza kutoka kwayo.
- Yapo maswali mengine yanayoulizwa katika maswali ya ufahamu ambayo yapo nje na ufahamu aliosoma.
- Maswali haya madhumuni yake ni kujaribu uwelewa wa mtahiniwa katika nyanja ya lugha ya Kiswahili.
VIDOKEZO!
- Baada ya kusoma kwa makini, atatakiwa kujibu maswali yanayohusiana na ufahamu aliousoma.
- Kumbuka asilimia kubwa ya maswali ya ufahamu majibu yake yamo katika ufahamu.
- Kutokana na neno ufupisho tunapata, ‘’fupisha’’ yaani punguza kitu kilichokua kirefu na kuwa kifupi na kinachoeleweka.
- Katika swali la ufupisho, mtahiniwa hupewa ufahamu mrefu asome na kuuelewa.
- Baada ya kusoma na kuuelewa kwa mapana, atatakiwa kufupisha maneno aliyoyasoma hadi kiwango ambacho ataulizwa katika maswali.
- Sehemu ya matayarisho pia huitwa nakala chafu.
VIDOKEZO!
- Mtahiniwa anatakiwa kuzipanga hoja zake zote zilizo bayana.
- Unapoambiwa kua hio ni nakala chafu, ina maana ya kua hio ni nakala inayotengenezwa ili kutaarisha nakala iliyo safi.
- Hivyo basi itamhitaji mtahiniwa kupiga mstari wa mshazari (/) ili kuyafuta yale aliyoandika.
- Sehemu ya matumizi ya lugha ndiyo inayobeba asilimia kubwa ya alama katika mtuhani wa karatasi ya pili.
- Hua na alama zinazofikia arobaini (40).
- Maswali ya matumizi ya lugha humzindua mwanafunzi kwa kuuliza maswali yanayogusia muundo na msingi wa lugha ya Kiswahili.
VIDOKEZO!
Baadhi ya maswali ni kama vile;- Sauti za matamshi – huuliza kuhusu suati za matamshi, sifa zake na sehemu zipotamkiwa.
- Methali na nahau. – huuliza methali ili mtahiniwakukamilisha. Pia huuliza maana za nahau.
- Umoja na wingi—huuliza kuhusu kugeuza sentensi katika umoja au wingi.
- Uakifishaji.—hutahini kuhusu alama za uakifishaji na matumizi yake.
- Maswali ya misamiati.—huuliza maneno au majina mapya na maana yake.
- Ukubwa na udogo.—humhitaji mtahiniwa kubadilisha sentensi katika ukubwa au udogo.
- Aina za maneno.—huuliza kuhusu aina nane za maneno ; nomino, kivumishi, kihusishi,kihisishi, kielezi,kiunganishi, kiwakilishi na kitenzi.
- Ukanusho na kinyume.-- kukanusha ni kukataa na kinyume ni tofauti ya jambo.
- Ngeli za majina. – huuliza kuhusu ngeli faaafu za majina. Ujuzi wa ngeli sahihi humsaidia mtahiniwa jinsi ya kuzungumza kwa ufasaha.
- Uchanganuzi wa sentensi. – humhitaji mtahiniwa kuivunja sentensi ili kupata aina za maneno kwa kutumia mbinu kama vile; matawi, mtari, mshale na jedwali.
- Mnyambuliko wa vitenzi n.k – huuliza kuhusu jinsi neno linavyoweza kunyambuliwa kwa vitenzi katika kauli kama vile; kutenda, kutendana, kutendatenda, kutendua, kutendwa, kutendeka ,kutendesha , na nyengine nyingi.
- Uyanishaji – humhitaji mtahiniwa kuirudisha sentensi kutoka hali ya ukanusho hadi hali ya sawa.
- Isimujamii ni taaluma inayochunguza lugha na matumizi yake katika jamii.
- Lugha huweza kuchunguzwa kutokana na utofauti wake na lugha nyenginezo baada ya kufanya ulinganishi.
- Vilevile isimujamii huchunguza ni kwanini mawasiliano baina ya watu yanaweza kufanyika ila watu wasielewane.
VIDOKEZO!
- Mtahiniwa anaweza kupewa dondoo kisha akaulizwa abainishe sajili, hii ina maana ya kua, aeleze ni sehemu gani ambapo lugha hio inatumika.
- Ni vizuri atoe sababu kutokana na dondoo hio.
- Iwapo atasema sajili ni ya sokoni, basi mtahiniwa anafaa kuonyesha ithibati kutoka kwenye kifungu cha maneno alichopewa na kuthibitisha jibu alilotoa.